Aston Villa Yawalaza Chali Chelsea.

Aston Villa wanajambo lao kwenye dirisha la usajili Januari hii. Hakika, Steven Gerard anapata msaada mkubwa kutoka kwa viongozi wa klabu hiyo. Chelsea wamelala chali!

Villa wapo mbioni kukamilisha usajili wa Lucas Digne akitokea Everton. Ni dhahiri, uhusiano wa Digne na kocha wa Everton, Rafael Benitez ulishavunjika. Kwa sababu hizi, Digne aliamua kumueleza wazi Benitez kuwa anataka kuondoka klabuni hapo mwezi huu.

Miongoni mwa timu zilizokuwa zikimuwinda Digne ni Chelsea na West Ham United. Everton waliweka wazi, Digne hatotolewa kwa mkataba wa mkopo, yeyote anayemtaka amsajili kwa mkataba wa moja kwa moja.

Lucas Digne

The Blues na The Hammers, wote wameshindwa kufua dafu kwa Aston Villa. Lucas Digne anakuwa ni usajili wa pili kwa Villa baada ya Philippe Countinho.

Kufuatia kukamilika kwa usajili huu, huenda Lucas Digne akawepo kwenye kikosi kitakacho chuana na Manchester United wikiendi hii.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe