Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amekanusha uwezekano wa Eddie Nketiah kuihama klabu hiyo katika dirisha la usajili la mwezi Januari.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 yupo katika miezi sita ya mwisho ya kandarasi yake kwenye Uwanja wa Emirates na anaaminika kuwa kwenye mazungumzo ya kuhamia Crystal Palace.
Kuelekea mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la EFL dhidi ya Liverpool, Arteta alisisitiza kwamba Muingereza huyo hataelekea kwingine wakati wa majira ya baridi.

“Hali ni kwamba Eddie ni mchezaji wetu na Eddie atasalia hapa kwetu. Ni mchezaji wetu na yuko chini ya mkataba, kwa hivyo atakuwa nasi,” Arteta
Nketiah ameona nyavu mara matano kwenye mechi tatu za Kombe la EFL msimu wa 2021-22, lakini amecheza dakika 38 pekee kwenye Ligi Kuu msimu huu.
Kinda huyu wa Uingereza anajivunia jumla ya mabao 18 na asisti moja katika mechi 72 akiwa na Arsenal akitokea akademi yao ya Hale End.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

