Tetesi zinasema, Borussia Dortmund wanatazamiwa kukutana na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland wiki ijayo huku wakijaribu kujua mipango ya mchezaji huyo kuhusu mustakabali wake.
Sevilla wametuliza nia yao ya kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial kwa vile hawawezi kumudu matakwa ya Manchester United ya kumsajili kwa mkopo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26.
Kiungo wa kati wa Paris St-Germain Georginio Wijnaldum amekuwa akihusishwa na Newcastle United lakini mchezaji huyo hana nia ya kurejea katika klabu yake ya zamani.

Meneja Jose Mourinho amewasiliana na kiungo wa kati wa Spurs Tanguy Ndombele katika juhudi za kumshawishi kiungo huyo kujiunga na klabu ya Roma, huku klabu hiyo ya Italia ikitaka mkataba wa mkopo na chaguo la kumnunua.
Tetesi zinasema, Marcus Rashford, 24, anatarajiwa kufanya mazungumzo na Manchester United kuhusu kandarasi mpya, huku mazungumzo yakitarajiwa kuanza kabla ya mwisho wa msimu huu.
Crystal Palace wako kwenye mazungumzo ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Eddie Nketiah kutoka Arsenal, huku kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ikimalizika msimu wa joto.
Tetesi zinasema, Brighton na Newcastle United wanapanga kujaribu kumsajili beki wa Argentina Marcos Senesi, 24, kutoka klabu ya Uholanzi ya Feyenoord.

Tottenham wanataka kusajili beki wa kulia, kiungo na mshambuliaji wakati wa dirisha dogo la usajili la Januari baada ya mkutano kati ya meneja Antonio Conte, mwenyekiti Daniel Levy na mkurugenzi mkuu wa soka Fabio Paratici.
Tetesi zinasema, Winga wa Ufaransa Kingsley Coman, 25, anakaribia kusaini mkataba wa mpya na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich.
Chelsea wanafikiria kumrejesha nyumbani beki wa kulia wa Uingereza Dujon Sterling, 22, kutoka kwa mkopo wa msimu mzima huko Blackpool lakini wana hadi Januari 14 kufanya hivyo.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

CHEZA HAPA

