Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu

Atletico Madrid wameripotiwa kuwa tayari kumchukua kiungo wa Milan Hakan Calhanoglu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uturuki, ambaye alicheza mechi waliyopewa kichapo cha 3-0 dhidi ya Italia Ijumaa, alikuwa na ushawishi mkubwa kuisaidia Milan kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2020-21, huku Milan akimaliza nafasi ya pili kwenye Serie A.

Calhanoglu alichangia asisti 10 na mabao manne katika michezo 33 ya Serie A, lakini amechagua kutosaini mkataba mpya na Milan, na tayari walimpa mkataba mpya ambao hajasaini.

Mchezaji huyo wa miaka 27 anatajwa kuwa tayari kuhama bure kama wakala huru kabla ya 2021-22 na ripoti za Marca ni kuwa Atletico Madrid wamejiunga kuisaka saini yake.

Nyota huyo wa zamani wa Bayer Leverkusen alipokea ofa kutoka Qatar na akafafanua kuwa yuko tayari kuhamia Galatasaray kabla ya mchezo wa ufunguzi kwenye Mashindano ya Uropa.

Los Rojiblancos wameripotiwa kupigana dhidi ya vilabu vya Ligi Kuu kwa saini ya Staa huyu.


 

SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

INGIA MCHEZONI

2 Komentara

    Hatariii

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

Acha ujumbe