Mashindano ya French Open 2021 yamemalizika rasmi baada ya mchezo wa Novak Djokovic vs Stefano Tsitsipas kwenye fainali.
Licha ya kuanza mchezo kwa kupoteza seti 2 za mwanzo, Djokovic alirejea uwanjani na kupindua meza. Hakika ameonesha ubora wake kama mchezaji namba 1 kwa ubora duniani (wanaume).
Mpaka mchezo unamalizika, Novak Djokovic alikuwa na matokeo ya seti 6-7 (6-8) 2-6 6-3 6-2 6-4. Matokeo haya yanamfanya Djokovic kuwa na taji 1 pungufu ya rekodi inayoshikiliwa na Roger Federer na Rafael Nadal (20).
Baada ya kumtoa Nadal kwenye nusu fainali ya French Open, Djokovic anakua mchezaji wa kwanza (mwanaume) kushinda mataji yote 4 ya Grand Slams mara mbili. Endapo Djokovic atafanikiwa kutetea taji lake la Wimbledon, ataifikia rekodi ya Federer na Nadal (mataji 20 ya Grand Slam).
SHINDA TSH 150,000,000/=
Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑
magdalena
Safi sana
Hope mwaikuka
Imekaa gud