Aubameyang : Sina Matatizo ya Moyo, Niko Salama.

 

Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang anasema moyo wake uko sawa kabisa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, wakati PSG, Juventus na AC Milan wakiulizia upatikanaji wa mshambuliaji huyo.

 

Aubameyang, 32 alirejea London kutoka Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON 2021 kwa uchunguzi wa kimatibabu baada ya kugundulika kuwa na vidonda vya moyo kufuatia kipimo cha virusi vya corona.

Kufuatia uchunguzi wa kimatibabu, Aubameyang aliandika kwenye Instagram: “Nilirudi London kufanya uchunguzi wa ziada, na nina furaha sana kusema kwamba moyo wangu uko sawa kabisa na ni mzima kabisa!!

“Nashukuru sana jumbe zote za siku chache zilizopita na tayari nimerejea.”

Bado haijaamuliwa iwapo nahodha huyo wa Gabon atarejea Cameroon kwa Kombe la Mataifa ya Afrika, huku The Panthers wakipangwa kuvaana na Burkina Faso Jumapili katika hatua ya 16 bora. Aubameyang bado hajashiriki michuano hiyo nchini Gabon.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe