Tetesi zinasema, Real Madrid inakaribia kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe ,23, kutoka PSG , na atajiunga kama mchezaji huru wakati mkataba wake utakapoisha.
Paris St-Germain iko katika mazungumzo ya kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Tanguy Ndombele, 25, kwa mkopo . Ndiye mchezaji aliyenunuliwa kwa kitita kikubwa wakati akijiunga na klabu hiyo 2019 kwa dau la £53m.
Tetesi zinasema, Sevilla bado inataka kumsajili mshambuliaji wa Man United na Ufaransa Anthony Martial , 26, kwa mkopo licha ya ombi lao kukataliwa.
Tetesi zinasema, Newcastle United wamewasilisha ombi la dau la £14.5m kumnunua beki wa kushoto wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Mitchel Bakker, 21.
Tottenham inafikiria kuwasilisha ombi la kumnunua kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast franck Kessie, 25 wakati wa dirisha la uhamisho.
Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba hajaiambia Manchester United iwapo anataka kusalia katika klabu hiyo zaidi ya mwisho wa msimu huu wakati kandarasi yake itakapokamilika.
Timu mbili , ikiwemo moja nchini Ujerumani , zina hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele kwa mkopo baada ya mchezaji huyo mweye umri wa miaka 24 aliyejiunga na Barcelona kwa dau la £135m 2017, kuambiwa kuondoka kwasababu hataki kutia Saini kandarasi mpya.
Beki wa Italia mshindi wa kombe la Dunia Fabio Cannavaro, 48, amehojiwa na Everton kuhusu wadhfa wa ukufunzi ulio wazi katika timu hiyo. Cannavaro alikuwa anakinoa kikosi cha China cha Guangzhou Evergrande hadi mwezi Septemba.
Mkufunzi wa Watford Claudio Ranieri amethibitsha kwamba klabu hiyo ipo katika harakati za kumsajili winga wa Bordeaux na Nigeria Samujel Kalu kwa dau la £3m, na beki wa Liverpool Nathaniel Phillips, 24.
Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.
CHEZA HAPA