Everton Wamfanyia "Interview" Fabio Cannavaro

Klabu ya Everton imefanya mazungumzo na  Fabio Cannavaro kuhusu kuchukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo inaoneka kwenye mazungumzo hayo wamevutiwa nae kuweza kuchukua mikoba iliyoachwa na Rafa Benitez.

Duncan Ferguson hivi karibuni amechaguliwa kuingoza timu hiyo kusimamia michezo ya hivi kribuni, hakuna ishara inayoonesha kuwa kama kuna uwezekano wakumpata mrithi wa Benitez hivi karibuni.

Everton
Everton

Hivi karibuni makocha kadhaa wamekuwa wakihisishwa na klabu ya Everton, huku walifanya mazungumzo na kocha wa Derby Wayne Rooney na Frank Lampard, huku wakizuia kufanya mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya Ubelgiji na chama cha soka Cha nchi hiyo.

Fabio Cannavaro ambaye alianza kazi yake kwenye klabu ya Ah-Ahli july mwaka 2013, awali aliweza kukaa kwenye klabu kwa muda wa miaka miwili awali kama muwakilishi wma baadae kama mshauri wa mipango.

Mwaka 2014 aliweza kuondoka falme za kiarabu na kwenda china kwenye klabu ya Guangzhou Evergrande Taobao, kipindi ambacho China waliaza kufanya uwekazaji wa wachezaji wa kigeni kwenye ligi yao.

Hata hivyo hakuweza kukaa kwa muda mrefu nchini China baada ya michezo 22 tu alitimuliwa, na akapata tena kazi nchini Saudi Arabia kwenye klabu ya Al-Nassr FC nako alitimuliwa baada ya miezi minne.

Mwaka 2016 alirudi tena China na aliacha kazi baada ya matatizo ya kifedha ya klabu, mwaka 2019 alifundisha timu ya taifa China kati mwezi march hadi april 2019.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe