Nyota huyo wa Ivory Coast na klabu ya Manchester United anategemewa kuwa nje ya kikosi hicho kwa kipindi chote cha msimu huu baada ya kupata majeraha kwenye mechi yake ya kwanza msimu huu huku akiwa ametoka benchi kutokana na majeraha ambayo yalimfanya akae nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.
Mbali na kukosekana msimu mzima pia, nyota huyo atakosa kushiriki michuano ya mataifa ya Afrika inayotegemewa kuanza kutimua vumbi huko nchini Misri mapema mwezi wa sita. Kutokana na majeraha yake hawezi kuwepo ndani ya kikosi cha timu hiyo.
Bailly aligundulika kwamba ameumia kifundo cha mguu wake baada ya kukutana na nyota wa Chelsea, Mateo Kovavic wakati wakigombea mpira. Baada ya kipindi kifupi nyota huyo alichezewa vibaya na kutolewa nje ya uwanja mapema kipindi cha pili jambo ambalo litamfanya kuwa nje kwa msimu mzima kwa sasa.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa anarejea uwanjani ikiwa ni mapema tu toka mara yake ya mwisho alipofanya hivyo pale Februari 3 na ni kama bahati mbaya kwake kurudi majeruhi tena ikiwa ni wakati ambao alianza kuonesha tumaini kikosini kwake.
Ivory Coast wapo katika kundi gumu ambalo kwa hakika wanahitaji uwepo wa nyota wazoefu kama Bailly ili kuwasaidia kusonga mbele zaidi kwenye michuano. Kundi lao lina timu za Morocco, Afrika Kusini na Namibia; hakika ni kundi ambalo lina nyota wengi sana na vikosi vinavyojiweza katika kipengele cha uwezo na uzoefu.
Jopo la madaktari laanika wazi kwamba majeraha aliyoyapata nyota huyo ni makubwa na hayawezi kumpa nafasi ya kurejea uwanjani haraka maana eneo aliloumia mara nyingi huchukua kipindi kirefu kuwa uimara. Mbali na hilo, michuano mingine iliyo mbele yake hususan ile ya Afrika hawezi kabisa kuishiriki.
Mbali na kuwa hiyo ni bahati mbaya kwa kikosi cha Ivory Coast kumkosa nyota huyo, pia United watamkosa nyota huyo huku wakiwa na uhitaji wa walinzi wa kati baada ya Smalling na Jones kuwa majeruhi. Hivyo, kocha alibakiwa na chaguo hilo kama mbadala wa walinzi hao wa kati na hadi sasa amebakiwa na wawili ambao ni Lindelof na Rojo katika nafasi hiyo na ndiyo atakaosafiri nao kwenye mechi mbili zilizosalia.
Upande huo wa Gunnar wapo nyuma kwa alama tatu kutoka kwa wale anaofukuzana nao ili kupata nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya klabu bingwa msimu ujao. Hivyo kwa sasa wanajitahidi ili aibu hiyo iwapitie mbali na wasiweze kupoteza ubora wao kwa kukaa nje ya michuano hiyo.


isha
Pole sana kaka
Povel
Duh majanga