Mshambuliaji wa Brescia, Mario Balotelli amechoshwa na maneno maneno juu yake kama anaendelea na mazoezi au lah!
Inakumbukwa mara Bolotelli aliripotiwa kurejeshwa nyumbani alipowadia mazoezini siku kadhaa zilizopita. Balotelli alinukuliwa akiwaambia waandishi kuwa waandika habari zao kuwa hafanyi mazoezi.
Wakati kasheshe likiendelea kubamba mtaani juu ya jamaa huyu kufanya au kutofanya mazoezi, mshambuliaji huyu ameamua kuja juu na kujibu kuwa yeye anafanya mazoezi na kama vipi “Mje mjionee wenyewe nikifanya mazoezi”

Staa huyu na klabu yake bado wanaripotiwa kuwa kwenye mgogoro, wakati klabu ikitajwa kuwa haijamruhusu kufanya vipimo vya Corona na pia kutomlipa mshahara wake wa mwezi Machi.
Balottelli aliamua kuchapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu hali inayoendelea na maswali juu yake.
“Inatosha sasa kuniuliza kuhusu kwenda au kutokwenda mazoezini, ninaenda mazoezini, nimekuwa kule wakati wote, inatosha maswali haya tafadhali.”
“Kama mnataka kuthibitisha mje mjionee wenyewe. Nina vipindi viwili hadi Jumapili, asubuhi na jioni. Njoo hapa utaniona.” -Mario Balotelli
Chapisho lake limeambatana na picha yake akiwa anavuja jasho baada ya mazoezi kadhaa.


Caroline
Balotel ni mkorofi jamani.
Ernest
Huyu jamaaa soka lipo mguuni sema tuu nae nidhamu yake na dharau ndo vinamrudisha nyuma
Theonestina
Yeye no mtu mzima hivyo anajua wajobu wake Kama nilazima afanye mazoezi
Ester jackson
Ballotel anajiamini sana na Mpira anajua ila anajeuri sana huyu
felister
ni lazima mpaka watu wakuone Kama unafanya mazoezi punguza ukorofi ballotel
Gabriel
Balotelli n mchezaji mzur ila ukimtibua n mkorofi
Povel
Duh thnks meridian bet tz kwa update zamichezo
Genia Sikaluzwe
Daaaah hatari Sana hiyo
Frank Patrick
Balloteli negativity za watu juu yake zinamuathiri sana
Lydia Emmanuel Magoti
Daa Balotelli anajua ila ana yumba wapi
Elika
Wanamuonea ila maneno sio mazuri..ballotell fanya kile unachojisikia
Khadija
Balotelli yupo vzr#meridianbettz
Dorophina
Baloteli ni mchezaji mzuri ila mkorofi sn
Neema hassan
Baloteli mchezaji mahiri aache jeuri..
Hope mwaikuka
Simkubal wala nn
Christopher
Dah huyo jamaa kashindikana
Hidaya
Jamaa anajua sana sema ukorofi upo kwenye damu
isha
Balotelli ngenge za nini fanya mazoezi tukuone
Aziza mushi
Balotel ni mchezaji mzuri Sana Ila sasa ujeuriii.
David Pere
Huyu no mcheaji ambaye ni mwehu na ni mjinga namba moja dunian
Evaluziga
Kweli balotel ni mkolofi
Tahiya
Jamaa unazingua sana sisi mashabiki tumechoshwa na drama zako
Rehema
Yuko vizuri sana
Mwanaidi
Balotelli ni mzinguaji bhn
Hamidu
Talent player#meridianbettz
Amani
nidhamu yake na dharau ndo vinamrudisha nyuma# meridianbettz
Furahav
Anazingua huyu kiande.
Zeiyana
Balotelli mzee wa matukio hata ukifanya haonekani kama hanafanya
Theckla
Balotelli ana kiburi sana
Shafii
Huyu jamaa kila leo anazungumziwa yeye tu habadiliki hata umri ukimtupa mkono
Sadick
Kama ni ndoa tungesema ipo hatarini kuvunjika! Balotelli bado dunia inasubiri kuona kipaji chake halisi#meridianbettz
Mwajuma
Kweli kizuri akikosi kasolo
Salma
Nimzuri ila anazingua
lombo
mmh kama mambo magumu fanya mpango wa kuhama tu ndugu maana marumbano kweny kaz si mazur
Emmy cleopa
Yuko vizur sana
Magdalena
Balotelli unaniangusha kwanini uachi utukutu
warda
Mie namkubali sana huyu jamaa#Meridianbettz
Agness
Nimchezaji mzuri mengine ni madhaifu ya kiubinaadamu
Issa
Baloteli mzuri sema vituko vimezidi uwanjani