Barca Wanamchongo Wa Januari Kwa Man United.

Uhalisia ni kwamba, Barcelona hali ni mbaya. Kuanzia uchumi mpaka uwezo uwanjani. Barca wanakazi ya kufanya msimu huu.

FC Barcelona ni miongoni mwa vilabu vikubwa kwenye ulimwengu wa soka. Wachezaji wengi wanatamani kucheza Camp Nou lakini, ni Barca ya namna gani hasa inayowavutia wachezaji. Ni ile iliyokuwa inatwaa mataji kila msimu au ni hii inayotepeta kwa misimu kadhaa sasa.

Wahenga wanasema, ‘kufa kufaana’. Barcelona wanamchongo wa januari kwa wakubwa wenzao, Manchester United. Barca inakila sababu ya kumpata mrithi wa Sergio Aguero baada ya mchezaji huyo kustaafu soka kwa sababu za kiafya.

Sergio Aguero

Kustaafu kwa Aguero, kunaibakiza Barcelona ikiwa na washambuliaji wawili tu (Braithwaite na Luuk de jong) ambao, wote hawajaonesha uwezo wa kumshawishi Xavi Hernandez kuwaamini.

Kwa sababu hiyo, inaripotiwa kuwa, FC Barcelona inamuwinda Anthony Martial ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu kwenye kikosi cha United kwa muda sasa. Inasemekana, Martial yupo tayari kuondoka United mwezi Januari ili kupata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

Matakwa ya Martial na Barca, yanafanana. Swali ni, Je Barcelona wanapesa ya kuwalipa Man United? Pesa inaweza ikawa kikwazo lakini, mchongo wa Barcelona ni kuwapa United nafasi ya kuchagua mchezaji mmoja kati ya – Dembele, Lenglet, Coutinho na De Jong ambaye watabadilishana na Martial.

Anthony Martial

Miongoni mwa wachezaji wanaopendekezwa, Dembele, Coutinho na De Jong wamekuwa wakihusishwa na United kwa muda mrefu bila mafanikio. Kwa United ya sasa, huenda De Jong ndio akapewa nafasi kubwa ya kukubaliwa United kwa vile anauwezo mkubwa wa kuwa mrithi wa Paul Pogba kwa miaka mingi ijayo. Hakika, huu ni mchongo wa wakubwa.


KUWA BINGWA MSIMU HUU WA SIKUKUU NA OCEAN CALL

Nani hapendi kuwa bingwa na kujishindia mkwanja wa kusahato kuelekea katika sikukuu wiki hii. Mchezo wa Ocean Call kutoka kasino maridhawa za meridianbettz unakupa kila sababu ya kuifanya siku kuu yako kuwa ya kuvutia zaidi.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.