Inaweza isizungumziwe moja kwa moja lakini kauli na matendo ya viongozi wa juu zikaonesha nia dhahiri na kwa namna wanavyohitaji uwepo wa mchezaji huyo katika kila mechi waliyonayo mbeleni pamoja na kwamba akiwa kama binadamu anapaswa kupata angalau mapumziko ili kukabiliana na majukumu mazito ya mechi zinazomjia mbeleni.
Wana biashara nzito mbeleni ndani ya ligi na kwenye michuano ya klabu bingwa kwa kuhitaji kupata ushindi kwenye mechi zao hizo. Ushindi wao wa kwanza ni ndani ya ligi wakisubiri kukabiliana na Villareal na kwenye mechi hiyo wanahitaji alama kwa namna yoyote ile ili kujiimarisha zaidi kileleni mwa ligi hiyo.
Lakini pia wana mechi ngumu mbele ya Atletico Madrid kwenye ligi yao, mechi ambayo bado wanahitaji kushinda ili waweze kuweka angalau tofauti kubwa ya alama kati yao na Atletico ambaye ndiye anafuata kwenye uongozi huo. Jambo hilo linaonekana kumsumbua sana akili kocha juu ya namna ya kuwapumzisha wachezaji wake.

Ni kitu ambacho hakifichiki kwamba Messi ndiyo nguvu ya kikosi hicho ilipo na kukosekana kwake ni janga kwa kikosi hicho na hata imani ya mashabiki hushuka juu ya kikosi chao kutoka na ushindi kwenye mechi husika.
Kutokana na uzito wa mechi zinazokuja mbeleni, kulikuwa na namna mchezaji huyo angeweza kupewa angalau mapumziko lakini kutokana na umuhimu wa kila mechi inaonesha wazi ni jambo linalomshinda Valverde afikirie juu ya mechi ipi anaweza kumpumzisha mchezaji huyo ili angalau waweze kuandaa mashambulizi sahihi kwa mechi kubwa zinazowakabili ndani ya mwezi huu.
Wana kikosi kipana lakini nafasi yake haiwezi kuzibika kabisa. Kwake amelipa jina wiki hili kwamba ni wiki la maangamizi kutokana na uzito wa mechi alizonazo na kila mechi iliyopo ni ngumu kwake kwa maana kwamba hata ule wakati wa kutulia na kujikusanya upya kwa mechi zinazofuata. Kwa mechi hizo kuna haja ya wachezaji tegemezi kupewa muda wa kupumzika.
Mechi ya muhimu kwake kwa sasa ni kati yao na Atletico na hiyo ni miongoni mwa mechi zinazohitaji ukaribu na uwepo wa kikosi chote ili kujihami zaidi kama mazingira yoyote ya kupoteza alama yatatokea. Hivyo, ni mtihani juu ya nani achukue nafasi yake ili aweze kumpa nafasi ya kupumzika kabisa.
Baada ya mechi yao hiyo watatakiwa kukutana na United ambapo watatakiwa kusafiri kuwafuata wazee wa Old Trafford ili kuhakikisha angalau wanaondoka na alama kwenye mchezo huo. Hadi sasa kocha anaona kabisa kuna uwezekano wakumtumia tena mchezaji huyo kwenye michuano hiyo wanahitaji kubaki katika uwezo wao wa mara zote hivyo nafasi ya Messi bado inatakiwa ili kuwapiku wapinzani wake.


Furahav
Messi ndo kila kitu barca.
Povel
Gud news