Kwa mujibu wa Alvaro Odriozola, mchezaji mwenzie Karim Benzema ndiye namba 9 bora duniani.
Karim alicheka na nyavu dakika ya 89 pale Santiago Bernabeu wakiwachapa 3-2 Huesca kwenye gemu ya La Liga.
Staa huyu alitia kazi na kutoa mchango wake muhimu katika magoli yote yaliyopatikana mapema kabisa kabla ya yeye mwenyewe kucheka na nyavu dakika za lala salama.
Benzema amewachapa magoli wapinzani wake wote 34 wa La Liga akiwa amejiandikia magoli yake 14 kwa msimu huu.

Licha ya kujua kuwa kuna mastaa washambuliaji kama Harry Kane, Luis Suarez, Robert Lewandowski, Edinson Cavani na hata Cristiano Ronaldo, bwana Odriozola anaona Benzema ndiye bora zaidi wa aina yake.


Povel tz
Gud update