Bournamouth Yatangaza kocha Mpya

Klabu ya Afc Bournamouth inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza imetangaza kocha mpya ambaye amechukua nafasi ya aliyekua kocha wa klabu hiyo ambaye alitimuliwa Scott Parker.

Klabu hiyo imemteua Gary O’neil kama kocha mkuu wa klabu hiyo kwa mkataba wa miezi 18 na kipengele cha kuongeza miezi mingine 12 ndani ya klabu hiyo inayoshika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.bournamouthKlabu ya Bournamouth ilifikia hatua ya kumtimua kocha wake ndani Scott Parker baada ya mfululizo wa matokeo mabaya katika michezo ya ligi ya kuu ya Uingereza na kocha O’neil akakaimu nafasi hiyo mpaka pale alipopewa mkataba wa kudumu.

Bournamouth ambao wamefanikiwa kupanda daraja msimu huu wakitoka katika ligi daraja la pili wanaonesha hawahitaji kushuka tena ndio maana walimuondoa kocha Parker mapema na kwakua walihitaji timu ipate matokeo mazuri na kuepuka kushuka daraja.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.