Bruno Fernandes Anataka Kubaki Man United

Nahodha wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ureno Bruno Fernandes amesema anahitaji kubaki ndani ya klabu hiyo kwa muda mrefu zaidi na hana mpango wa kutimka.

Bruno Fernandes ameweka wazi anahitaji kuwepo kwenye mradi wa klabu hiyo kwa mudamrefu zaidi,Huku akisema ameshakutana na mmiliki mpya ambaye pia amekutana wachezaji wote.bruno fernandesKumekua na taarifa zikiendelea kua nahodha huyo anaweza akaondoka klabuni hapo hivi karibuni, Lakini amekanusha taarifa hizo na kusema yeye mpango wake ni kuendelea kuwatumikia mashetani hao wekundu kwa muda mrefu zaidi.

Kiungo Bruno Fernandes ambaye kwasasa yupo kwenye kambi ya timu yake ya taifa ya Ureno amekua mchezaji muhimu sana tangu ajiunge na timu hiyo mwezi Januari mwaka 2020, Jambo ambalo limefanya uongozi wa klabu hiyo kuendelea kumuamini na hata kupelekea kocha Ten Hag kumpa kitambaa cha unahodha.

Acha ujumbe