Deco: Araujo Atasaini Mkataba Mpya Akitaka

Mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Barcelona Deco amesema beki wa klabu hiyo Ronald Araujo raia wa kimataifa wa Uruguay atasaini mkataba mpya akihitaji kwani upo tayari.

Deco amezungumza hayo baada ya kuulizwa juu ya mustakabali wa beki huyo ambaye inaelezwa mkataba wake unaelekea ukingoni, Hivo anapaswa kuongezewa mkataba mpya ili aendelee kusalia ndani ya klabu hiyo.decoMkurugenzi Deco amesema beki huyo anastahili kupewa mkataba mpya kwakaua wao kama klabu wanahitaji kuendelea kubaki na wachezaji wake wazuri, Hivo kipaumbele chao ni kumpa mkataba beki huyo mahiri klabuni hapo.

Taarifa mbalimbali zilieleza kua klabu ya Barcelona ilikua tayari kumuuza beki huyo katika dirisha dogo la mwezi Januari, Taarifa ambayo ilishtua mashabiki wengi wa klabu ya Barcelona kutokana na maamuzi ambayo yalitaka kufanywa na klabu yao.decoKlabu ya Barcelona inafahamika inapitia wakati mgumu kichumi jambo ambalo limepelekea klabu hiyo kutaka kuuza wachezaji wake muhimu ili kuweza kukaa swa kiuchumi, Hii inawezekana kwa kiwango kikubwa ni sababu ambayo ilipelekea klabu hiyo kufikiria kumuuza Araujo.

Acha ujumbe