Shirikisho la mpira wa miguu Ujerumani – Bundasliga na wanasiasa katika majimbo yote wamekubaliana kuwa na utaratibu sawa wa majaribio wa kuwarejesha mashabiki wa soka viwanjani.
Wanasiasa katika majimbo yote ya shirikisho la Ujerumani wamekubaliana kuwa na utaratibu sawa wa majaribio wa kuwarejesha mashabiki wa soka viwanjani pale ligi kuu ya soka ya Ujerumani-Bundesliga itakapoanza msimu mpya mwishoni mwa juma hili.

Kwa mujibu wa utaratibu ulioafikiwa viwanja vitaruhusu mashabiki kujaza asilimia 20 ya uwezo wake kwa kipindi cha wiki sita za mwanzo. Baada ya kipindi hicho mwishoni mwa Oktoba, mamlaka husika zitafanya tathmini ya majaribio hayo.
Mkuu wa shirikisho la soka la Ujerumani, DFB, Fritz Keller amesema amefurahishwa sana na uamuzi huo. Licha ya uamuzi huo wa nchi nzima, jimbo la kaskazini mwa Ujerumani la Schleswig-Holstein linajipanga kuruhusu mashabiki wa hadi asilimia 25 ya uwezo wa viwanja vyake.

Maamuzi hayo yanakuja katika muda muafaka ambapo Bundasliga na ligi nyingine za Ujerumani zikijiandaa kuanza kutimua vumbi kwenye viwanja visivyo na mashabiki.
Hata hivyo, bado haiko wazi iwapo vilabu vyote vya Bundasliga vitaweza kutekeleza hatua hiyo kwa wakati, wakati kipute cha Bundesliga kinapoanza Ijumaa wiki hii, ambapo mabingwa watetezi Bayern Munich wakifungua msimu kwa kukutana na Schalke 04.
Hali kuhusiana na maambukizi ya virusi vya corona, itatathminiwa tena mwishoni mwa mwezi Oktoba.
SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.


Sauda
Mashabiki ndo mpango mzima kwenye kandanda..
Povel
Habar njema kwa mashabik na wapenda soka ulimwenguni
Adelta
Habari njema kwa wapendwa wa soka@meridianbettz
Nasra
Soka inatupa burudani zaid
magdalena
afadhali wameruhusu mashabiki maana nilikuwa nawaza mpira bila mashabiki hauleti amsha amsha
Genia Sikaluzwe
Habari njema hizo kwa mashabiki
Zeiyana
Hi itakua vizuri hata ali ya uchumi hitapanda pia italeta hamasa kwa wachezaji
Shani
Motisha ya wa cheza ipo kwa washabiki!!
Shani
Motisha ya wachezaji ipo kwa washabiki hamsha amsha!!
Mwanahamisi
Soka inatupa burudani zaidi
Lydia Emmanuel Magoti
Niabari nzuri kwamashabiki kulusiwa kuingia uwanjani kwasababu Game bila masha biki hainogi kwaio nimwendo wa shangwe tuuu uwanjani
Antony Luseno
Hili ni jambo la kheri kwa wale wadau ambao wanapenda kwenda uwanjani
Njiku
Me naona wangetumia kwanza corona itoweke then mashabiki tupo tu
Dorophina
Bundesliga inarudi kwenye ubora wake hii itakuwa poa sana
Elika
Afadhar mashabiki wameruhusiwa.maana tulikuwa tuna wasiwasi labda ndo forever hiyo
Fatina
Ni Jambo zuri san kwa mashabiki
Caroline
Mashabiki wakiwa njiani raha Sana.wananogesha sana
Tatu
Hii habari nzuri kwatu mashabiki wa mpira
Mwajumah
Habari njema kwa mashabiki na wapenda soka#Meridianbettz
Ernest
Habari za kurudi kwa mashabiki uwanjani bado kizungumkuti sana kutokana na janga hili la Corona
Samira
Habari njema sana hii kwa mashabiki
Saupha mohamed
Jambo zuriii
Khadija
Habari njema kwa wapenda soka#meridianbettz
Hopemwaikuka
Habari njema sanaa hii
Latifa juma mohamed
Habari njema kwa mashabiki wa soka duniani.
Fatuma kasomo
Habar njm
Janeflora malisa
Nice
Gabriel
Maamuzi hayo yanakuja katika muda muafaka ambapo Bundasliga na ligi nyingine za Ujerumani zikijiandaa kuanza kutimua vumbi kwenye viwanja visivyo na mashabiki.
Hata hivyo, bado haiko wazi iwapo vilabu vyote vya Bundasliga vitaweza kutekeleza hatua hiyo kwa wakati, wakati kipute cha Bundesliga kinapoanza Ijumaa wiki hii, ambapo mabingwa watetezi Bayern Munich wakifungua msimu kwa kukutana na Schalke 04.
Issa
Ni freah kuleta mashabik
Sabrina
Itapendeza sana mashabiki wakirudi uwanjani walikua wanaisubiri hiyo burudani mda mrefu
Salma ngende
Vizuri
Rose kapinga
Wazo zuri
Samiah
Wazo zuri
Angelina
Habari njema
Mariam mtandama
Safi
Amiri Kayera
Litakua Jambo zuri
felister
habari njema kwa mashabiki