Buku Tatu ya Simba na Somo la Pricing Strategy

Kiingilio cha TZS 3000 katika mchezo wa Simba SC vs Biashara United ni sehemu ya mikakati mipya ya CEO wa klabu hiyo katika kujenga tabia ya wanachama kuingia kila mechi, kukuza mapato kutoka na wengi wataweza kuingia pia ni mkakati wa kuwasoma mashabiki wao au watazamaji kujua kujua shida ipo wapi kutoingia viwanjani katika zile mechi ambazo si za pressure sana ya matokeo.

CEO ni kama anaanza mikakati ya kuibrand klabu kwa pricing strategy. Akifanikiwa hili au kushindwa atakuja na mkakati mwingine ili kuendelea kutoa uzani sawa kwa mshabiki kwa kila mechi ya Ligi au kirafiki. Hapo atakuwa amefanikiwa katika ule mkakati alioutaja wa kukuza mapato (Revenue) kupitia rasilimali watu na vyanzo vingine.

Tuponde kwa dhana ya utani wa jadi na majigambo mengine lakini technically kuna somo kubwa linafanyika.

Soka letu sasa tunalitanua kutoa kwenye ‘pitch’ kuja nje kimkakati. Dakika 90 za uwanjani zinafanikiwa zaidi kutokana na kazi kubwa nje ambayo hugharimu muda , mali na akili za watu. Muunganiko kiutendaji ndio unaleta ufanisi wa dakika 90 zinazochezwa na timu. Kabla ya wachezaji kuingia uwanjani, CEO na line managers wake wote wanatakiwa kufanya kazi kubwa na yenye tija ili kuwapa ufanisi wachezaji. Malipo mazuri, bonus, kuhakikisha branding ya timu na klabu kwa ujumla ipo sawa, kufungua fursa kimasoko na mikakati kabambe ya kila uchao kuvuna rasilimali watu na kuongeza assets za klabu ili kukuza mtaji wake.

Moja ya mikakati hiyo ni hii ya kushusha kiingilio ili kupata volume kubwa ambayo ina faida nyingi kama lengo litafanikiwa. Kwanza kupanda mbegu ya wapenzi, wadau wa soka na mashabiki kwa ujumla kupenda timu yao au soka kwa ujumla. Lile vibe la uwanjani litamfanya na kesho kurudi na mwisho wa siku anapata ile addiction ya kuipenda Simba na soka kiujumla, hivyo kila mechi ataingia hata kama kiwango kitabadilika.

Hizi mechi zinatazamwa duniani kote . Wingi wa mashabiki viwanjani, unawavutia wawekezaji kuja kuwekeza kwakuwa wana uhakika na wingi wa rasilimali watu.


SHINDA NA MERIDIANBET!
Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.
Cheza Sasa.

33 Komentara

    Noma sana hiiiiiii THIS IS SIMBA next level. Twenden kwa MKAPA wakati wetu WAKUWAKERA

    Jibu

    ni noma sana apo hakuna kukosa ata kidogo

    Jibu

    Good news 👍😀 @meridianbettz

    Jibu

    Safi sana wanasimba

    Jibu

    Great madam CEO this plan of yours will make it!! !

    Jibu

    Ahsant sana meridianbet kwa taarifa

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Hii si ya kukosa

    Jibu

    Ipo poa hii

    Jibu

    Habari njema kwa mashabiki wa simba watawavuta mashabiki kwa wingi

    Jibu

    Wazo nzuri kaanza nalo CEO mpya wa klabu ya simba

    Jibu

    Mambo yamekuwa juju akuna Kama Simba tukutane kwamkapa ukaone watoto wanavyo ucheza mpila

    Jibu

    Mambo mazuri kwa club ya simba!!

    Jibu

    Hii itasaidia kwa ali ya uchumi ilivyo polomoka ila kwa Tanzania bado sana tiketi zitaendelea kuuzwa hivyo ivyo kwa bei ile ile kama hawajaweka uwangalizi kwa wauza tiketi wao

    Jibu

    Bora wameweka kiwango kidogo ili mashabiki tujumuike kwa wingi…simba hawanaga kazi mbovu wenyewe wanaridhika na kidogo wanachopata..sisi hatuna maneno eti kujaza uwanja..sisi tunaenda kuangalia mpira

    Jibu

    Sawa.hicho kiwango watu wengi watamudu

    Jibu

    CEO wa simba ni mwanadada mrembo na mwenye akili sana kitendo cha kushusha kiingilio hii itatufanya sisi mashabiki kuingia kwa wingi uwanjani pia umeisadia jamii kutoka hali yetu ya uchumi jinsi ulivyo sasa

    Jibu

    Sio kwa kiingilio hicho hakosi mtu apo#Meridianbettz

    Jibu

    Hapa nimekubali sana hili swala la kupunguza viingilio hasa katika kipindi hiki ulimwengu upo kwenye mapambano na Corona, Salute kwa CEO Mpya Madame mwenye Cv zake

    Jibu

    Mpira ni burudani simba wamejua kutufurahisha wapenzi wa mpira

    Jibu

    Mambo safi simbaa

    Jibu

    Hii si ya kukosa#meridianbettz

    Jibu

    🙊

    Jibu

    Iko pow

    Jibu

    C.E.O wa Simba n mrembo sana ninamatumain kazi yake itakuwa nzur

    Jibu

    Senzo atabak kuwa senzo

    Jibu

    Tunasubiri tuone

    Jibu

    3000 itapendeza

    Jibu

    Ni mwanzo mzur kwa CEO wetu mpya twende tukachangie klabu na uku tunapata burudani

    Jibu

    Goodnews

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Hili ni Jambo zuri

    Jibu

    hii si ya kukosa

    Jibu

Acha ujumbe