Cardetti: Ronaldinho ni Zaidi ya Messi

Kila mtu ana mtu anayemkubali zaidi, na inapofika nafasi ya kufananisha watu wenye uwezo na historia katika soka kila mmoja huwa na maoni yake! Kwa Martin Cardetti, kama angekuwa na nafasi ya kuchagua, angemchagua Ronaldinho dhidi ya supastaa wa Barcelona Lionel Messi!

Ronaldinho alifurahia na kupeta sana enzi zake za soka alipokuwa Barcelona, Milan, PSG na pia Brazil. Alifanikiwa kushinda Ballon d’Or mwaka 2005, Kombe la Dunia, Ligi ya Mabingwa na LaLiga ikiwa ni baadhi ya mafanikio yake kwenye soka.

Messi kwa upande mwingine, naye anachukuliwa kama mwanasoka wa kipekee na mwenye uwezo mkubwa kuwahi kutokea kwenye soka. Ana rekodi ya kushinda Ballon d’Or mara 6, akiwa na mataji ya La Liga 10 kibindoni, pia ana medali 4 ya Ligi ya mabingwa na mataji mengine mengi!

Lionel Messi na Ronaldinho walipata nafasi ya kucheza pamoja Barcelona, na kama unakumbuka vyema wakiungana na Neymar waliitwa wazee wamaajabu wa 3 kutoka Barcelona!

Cardetti: Ronaldinho ni Zaidi ya Messi
Messi na Ronaldinho walikuwa pamoja Barca.

Lakini kwa Cardetti, yeye anasema Ronaldinho ni mchezaji ambaye ameguswa na Mungu na kuwa na uwezo wa ajabu. Walikuwa timu klabu moja ya PSG kabla ya Ronaldinho kusepa kwenda Barcelona mwaka 2003.

Licha ya kutambua vyema mafanikio ya Messi, Cardetti yeye akiwa kama kocha angemchagua Ronaldinho kwa ubora dhidi ya Messi.

“Nilikuwa na Ronaldinho kwa mwaka mmoja, na ni mchezaji wa tofauti, ameguswa na mungu. Wakati wote alifurahia, akiwa na mpira alifanya vitu na kufanya mazoezi sana ili aweze kuonesha vitu hivyo kwenye mechi. Unamuona kuwanzia mazoezini, kwenye mechi na kila kitu anachokifanya anafanya tofauti na wengine.”

Cardetti anasisitiza kuwa yeye wachezaji wa aina ya Ronaldinho wanatokea mara chache sana kwenye historia ya soka, na anajivunia kuwa alikuwa karibu na mchezaji kama huyu. Ungekuwa wewe ni kocha, kati ya Messi na Ronaldinho nani angekufaa zaidi kwa uwezo wao? Achia komenti hapo chini

18 Komentara

    Ronaldinho yuko juu

    Jibu

    Kwangu Messi ni zaidi ya yeyote

    Jibu

    Ronaldinho kwangu zaidi ya Messi sababu huyu jamaa Ndio mwalimu wa Messi,

    Jibu

    Mesi ndio habari ya mjini

    Jibu

    Ronaldinho mnyama

    Jibu

    Gaucho mkali wao

    Jibu

    Fundi wa mpira

    Jibu

    Kipnd ronaldinho anafnya yke Messi alikuwa anatulia baada ya dinho kutoka Barcelona ndio Messi akapewa Jez ya dinho jamaa alikuwa kama Corona anatisha kwa kile kipnd

    Jibu

    Ronaldino was great, Messi is greater #meridianbettz

    Jibu

    Mess anajua.

    Jibu

    Messi kiungo

    Jibu

    Messi ndio mkali wao

    Jibu

    Gaucho namkubali sana

    Jibu

    dhino kabali yao

    Jibu

    Messi ndo baba lao

    Jibu

    mesi mkali hana mpinzani

    Jibu

    Messi Hana mpinzan..

    Jibu

    Messi mie namkubalii

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.