1. BARCELONA ILIISHIA KWA PEP GUARDIOLA

Alinufaika na portifolio la Johann Cruyff, akaja kumalizia alichoacha Frank Rijkaard, mfumo wa 4-3-3, La Masia iliyo bora sana, Pep kuanzia 2008 hakuwa hata na tabu ya kupanga kikosi kila kitu kilikuwa chepesi.
Messi, Xavi, Puyol, Iniesta, Pique, Etoo hawa wote wapo katika ubora, akabeba makombe zaidi ya 13, with the famous treble baada ya kumaliza muda wake aliondoka na Ferran Sorriano, Xiki Berigistain hawa wote walikuwa watu muhimu kwenye La Masia na eneo la ufundi la Barca, jumlisha na Rodolfo Borrel, kifupi Luis Enrique ‘Lucho’ alienda tu kumalizia ile project ila Barca ishajifia muda sana
2. SIR ALEX KAONDOKA NA UNITED YAKE

Babu alikuwa mtu wa matokeo, hakuwa Kocha mwepesi, alifundisha watu wagumu kama Eric Cantona, Roy Keane, Paul Ince na mabishoo kama David Beckham ila yeye alisimama kwenye misingi na alikuwa na absolute authority sio kama Ole Gunnar, kila siku kupamba wachezaji.
Waingereza wakiwa na nafasi kubwa zaidi, wale watoto wa Class of 92′ David Becks, Ryan Giggs, Gary Neville, Nick Butt na wenzao walikuja kumlipa sana kwenye treble ya 1999, yote yalitokana na mifumo sahihi ya soka
Bench lake alikuwa na watu kama Big Mike Phelan, alikuwa pia na scouting network ya ajabu sana, kikubwa Babu alicheza sana kamari, mfano ya Cristiano Ronaldo kinda wa miaka 18, Javier Chicharito, Wayne Rooney, Louis Saha na Nemanja Vidic, mkeka ulikuwa unatick sana
kocha baada yake sioni kama ni wabaya ila wanakwamishwa na mfumo wa sasa wa United, upo kibiashara zaidi.
3. PEREZ NA KIVULI CHA CRISTIANO RONALDO

Kumwachia mchezaji ambaye hazaliwi kila mwaka, na kila mahari duniani ni kamari mbaya sana, Cristiano bado alikuwa nguzo muhimu ndani ya Los Blancos.
Sokoni ni kazi kukuta mchezaji wa daraja lake, kama unamwachia Ronaldo inapaswa uwe na Messi, binafsi naona watapitia vipindi vigumu sana kama kile cha 2003-2009 mpaka hapo wapate mrithi sahihi. Zidane ni space goat tu kwasasa, hakuwa hata na maajabu makubwa Mido wa kifaransa, ila aliweka spirit ya Ronaldo na wenzake kupambana!


Kenani
Kwel kabisa
Frank Patrick
Kwa Man u hapo😂😂😂😂
Amani
Akuna kuchekana
JULIANA
Babu alikuwa mtu wamatokeo
Ernest Kimeru
It’s all about football!!!
Neema juma
Kwa kweliii
Nasra
Man Utd haahaahaa
Gabriel
Me Barcelona tu inanikosha
mwakalosi
mpira wa sasa umebadilika sana tuna mabishoo wengi kuliko wachezaji na pesa zimekuwa nyingi kuliko thamani ya miguu yao ndio maana sioni ajabu mpaka sasa messi na ronaldo kuonekana bora
Jenifer
Ngoja tu nicheke hahahhaha man
Sadick
Ni kawaida Kocha mahiri anapotoka ajaye anapata taabu kidogo kupata chemistry. Thanks #meridian
Warda
Coach wa Man U alitishaga sana
Lydia Emmanuel Magoti
Akuna kuchekana
Issa
Man u wana historia kubwa