Klabu ya Chelsea imeendele kuandamwa na majeraha ndani ya msimu huu wa mwaka 2022/23 baada ya jana kiungo Denis Zakaria kupata majeraha katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Fulham.

Klabu ya Chelsea jana imepoteza mchezo wake dhidi ya klabu ya Fulham kwa mabao mawili kwa moja mchezo uliopigwa katika dimba la Craven Cottage. Klabu hiyo imekua kwenye mfululizo wa matokeo mabaya kwani katika michezo yao nane ya mwisho wmepata ushindi mara moja.ChelseaKlabu hiyo imekua ikisumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu na katika mchezo wa jana kiungo wa klabu hiyo anayefanya vizuri Denis Zakaria kupata majeruhi na kuongeza idadi ya wachezaji majeruhi ndani ya klabu hiyo. Hali hiyo inaelezwa kupelekea klabu hiyo kutetereka kwa kiwango kikubwa.

Wiki moja iliyopita katika mchezo dhidi ya Manchester City klabu hiyo ilipata majeruhi wawili ndani ya timu hiyo ambao walikua Raheem Sterling na Christian Pulisic. Wachezaji hao walikua ni moja ya wachezaji wanaofanya vizuri ndani ya klabu hiyo.ChelseaDenis Zakaria ambaye alipata majeraha katika mchezo wa jana kati ya Chelsea na Fulham ambapo klabu hiyo ilipoteza mchezo huo, Bado taarifa rasmi ndani ya klabu hiyo haijatoka juu ya muda ambao mchezaji huyo atatumikia akiwa nje ya kiwanja.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa