Klabu ya Chelsea leo itashuka dimbani kumenyana na klabu ya Fulham katika mchezo wa ligi kuu ya Uingereza mchezo utakaopigw katika dimba la Craven Cottage jijini London.

Klabu ya Chelsea leo watakau ugenini wakikaribishwa na wenyeji wao klabu ya Fulham ambapo klabu hizo mbili zinatoka katika jiji moja la London. Hivo mchezo huo utakua mchezo wa derby kati ya miamba hiyo miwili kutoka jiji la London.ChelseaKocha Graham Potter atakua ana kazi kubwa ya kufanya katika mchezo wa leo kwani klabu hiyo imekua kwenye rekodi mbaya ya kupoteza michezo hivi karibuni, Kocha huyo anahitaji kupata ushindi leo dhidi ya Fulham angalu kurudisha hali ya kujiamini kwa wachezaji wake na timu nzima.

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kushinda mchezo mmoja pekee katika michezo yake saba iliyopita kwenye mashindano yote mpaka sasa, Hii ni ishara mbaya sana kwa klabu hiyo na mchezo wa leo utakua na umuhimu mkubwa sana kwa klabu hiyo wakihitaji kupata matokeo ya alama tatu.ChelseaKlabu ya Fulham wao  wanatarajiwa kua wapinzani wagumu sana leo mbele ya klabu ya Chelsea na hii ni kutokana na kiwango chao ambacho wamekua nacho siku za hivi karibuni. Klabu ya Fulham wao wamefanikiwa kushinda michezo yao mitatu ya mwisho ya ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa nafasi ya saba kwenye msimamo alama mbili juu ya vijana wa Graha Potter.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa