Klabu ya Atletico Madrid ipo kwenye mpango wa kumsajili Memphis Depay kutoka klabu ya Fc Barcelona ambaye amekua hapati nafasi kwenye timu hiyo chini ya kocha Xavi.

Klabu ya Atletico Madrid inataarifiwa kua ipo kwente mazungumzo na klabu ya Barcelona kwajili ya kupata saini ya mshambuliaji Depay. Klabu hiyo imepanga kuhakikisha inapata saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi.depayMshambuliaji Memphis Depay amekua kwenye wakati mgumu ndani ya klabu ya Barcelona baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi hicho chini ya mwalimu Xavi, Jambo lilimfanya mchezaji huyo nae kufikiria kwenda timu nyingine ili kuweza kupata nafasi ya kucheza.

Klabu ya Atletico Madrid inahitaji kupata mbadala wa mshambuliaji wake Joao Felix ambaye ametimkia klabu ya Chelsea kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu, Hivo klabu hiyo inamuhitaji Depay ili kuweza kuziba nafasi ya mchezaji huyo.depayMemphis Depay amekua akihitajika na vilabu kadhaa tangu dirisha kubw ala mwezi Juni huku vilabu vya Uingereza vikiongoza kwenye mbio, Lakini kwasasa klabu ya Atletico imeonekana kua na nguvu kuliko vilabu kutoka nchini Uingereza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa