Magolikipa Emiliano Martinez, Thibaut Courtois, Allison Becker,Ederson na Bounou wamechaguliwa kuwania tuzo ya golikipa bora wa mwaka ambayo inatolewa na FIFA.
Magolikipa hao watano wote wamefanikiwa kufanya vizuri mwaka jana kupitia klabu zao na timu za taifa, Huku Golikipa Emiliano Martinez akionekana kama yuko kwenye nafasi nzuri zaidi kushinda tuzo hiyo ubora waliokua nao kwenye michuano ya kombe la dunia.Golikipa Emiliano Martinez alikua na mwaka mzuri sana pale alipofanikiwa kuiwezesha Argentina kushinda taji la kombe la dunia nchini Qatar, Huku yeye akiwa kwenye ubora mkubwa na mhimili mkubwa katika ushindi wa timu hiyo pia akimaliza michuano hiyo kama golikipa bora wa mashindano.
Magolikipa wengine kama Courtois, Becker, Ederson, na Bounou wao pia walifanikiwa kufanya vizuri katika vilab vyao lakini katika michuano ya kombe la dunia ni Yousef Bounou pekee ambaye alifanya vizuri kuliko kwani alifanikiwa kuhakikisha timu yake ya taifa ya Morocco inafuzu hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza.Mpaka wakati huu magolikipa watano wamechaguliwa kuwania tuzo hiyo lakini Emiliano Martinez bado anaonekana kupewa nafasi kubwa ya kwenda kuchukua tuzo hiyo mbele ya magolikipa wote wanaogombania tuzo hiyo, Kwani golikipa huyo amefanya mambo makubwa haswa kwenye michuano ya kombe la dunia nchini Qatar.