Kocha wa klabu ya Napoli Luciano Spalletti amesema kua klabu ya Juventus ipo kwenye nafasi nzuri ya kuweza kutwaa taji la ligi kuu nchini humo maarufu kama Scudetto.
Klabu ya Juventus itakua na mchezo wa ligi hiyo siku ya ijumaa wakiwakaribisha klabu ya Napoli chini ya kocha Luciano Spalletti. Mchezo huo utapigwa katika dimba la Allianz ambapo klabu ya Juentus ndio watakua wenyeji wa mchezo.Kocha wa klabu ya Napoli Luciano ameamua kujibu kauli aliyoitoa kocha wa Juventus Massimiliano Allegri ambaye alisema Napoli ni trimu ambayo ni timu ambayo ipo kwenye nafasi nzuri zaidi msimu huu kubeba taji la ligi hiyo, Lakini kocha Spalletti akamjibu kwa kusema kua Allegri hataki kusema tu ukweli lakini ukweli ni kua klabu ya Juventus ipo kwenye nafasi bado ya kuweza kubeba taji la ligi hiyo.
Kocha Allegri amekua akisema mara kwa mara kua malengo ya klabu ya Juventus msimu huu ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kumaliza nafasi nne za juu ili kushiriki ligi ya mabingwa barani ulaya, Lakini Kocha Luciano Spalletti amempinga Allegri kwa kusema anadanganya kwani klabu kama Juventus haiwezi inaweka mipango ya nafasi ya nne na sio ubingwa kwani klabu hiyo inafanya uwekezaji mkubwa.Klabu ya Juventus imefanikiwa kushinda michezo nane ya ligi kuu ya Italia mfululizo bila kuruhusu, Kitu ambacho kimewafanya kusogea hadi nafasi ya pili ya msimamo wa ligi hiyo na ndipo kocha Spalletti alipoiona nafasi ya klabu ya Juventus kwenye mbio za ubingwa.