Chelsea inaripotiwa kuanza mazungumzo na nyota wao N’Golo Kante juu ya mkataba mpya katika miezi ijayo.
Hatma ya staa huyu wa miaka 30 huko Stamford Bridge ilianza kuwa katika sintofahamu msimu wa joto uliopita, lakini mwishowe alibaki na Chelsea na kufanikiwa kufanya vyema huko, akicheza mechi 48 katika mashindano yote mnamo 2020-21.
Kante amebakiza miaka miwili tu katika makataba wake wa sasa. Kwa mujhibu wa chanzo cha habari za michezo toka Italia, wamiliki Chelsea wanapanga kufungua mazungumzo ya mkataba mpya na mshindi huyu wa Kombe la Dunia katika miezi michache ijayo.

Taarifa zinadai kwamba kulikuwa na ofa mbili kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa wakati wa usajili wa msimu uliopita wa kiangazi, lakini alitaka kubaki na klabuni hapo.
Sasa Chelsea ni wanadaiwa kuwa wanataka kumzawadia N’Golo Kante, ambaye kwa sasa anaiwakilisha nchi yake kwenye Mashindano ya kimataifa EURO2020.
Kante amecheza mechi 218 kwa Blues tangu alipowasili kutoka Leicester City mnamo 2016.


