Chelsea wapo tayari kufanya mpango juu ya uhamisho wa beki wa Bayern Munich David Alaba kwa dirisha la usajili la mwezi Januari.

Licha ya kuendelea kuwa sehemu muhimu dimbani Allianz Arena, mkataba wa Alaba unapaswa kumalizika mnamo 2021, ambayo bila shaka imevutia nia ya kutaka kuinasa saini yake.

Liverpool, Manchester City, Real Madrid na Barcelona wote walikuwa wanahusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria wakati wa msimu wa kiangazi.

David Alaba

Hata hivyo, kwa mujibu wa AS, Chelsea inaweza kuwasilisha ofa rasmi ya kumtaka nyota huyu mnamo Januari, licha ya mchezaji huyo wa miaka 28 kuweza kuwa sokoni kama mchezaji huru ikiwa hatasaini mkataba na kusalia klabuni hapo hadi mnamo 2021.

Ripoti hiyo zinadokeza kwamba The Blues wanataka kuona kama Bayern wanaweza kumuachia kwa bei ya bei ya chini, badala ya kuwapa Mabingwa muda zaidi wa kukubali masharti mapya na mchezaji huyo.

Mazungumzo kati ya Bayern na Alaba yanadaiwa kusimama na Bayern hawajajiandaa kukidhi mahitaji yake ya mshahara.


 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Alaba, Chelsea Watamuweza David Alaba?, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

13 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa