Winga wa Ubelgiji, Eden Hazard anakabiliwa na janga jingine na atalazimika kuwa nje ya uwanja baada ya kupata jeraha la paja katika mchezo wa nyumbani wa Real Madrid waliopoteza dhidi ya Alaves Jumamosi.

Mchezaji huyo wa miaka 29 ameonekana katika mechi sita tu za msimu huu baada ya changamoto za majeraha na kupatikana na maambukizi ya corona mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa chapisho la Daily Mail , Hazard, ambaye alilazimika kuondoka mchezoni baada ya dakika 28 tu, alipimwa kipimo cha ultrasound siku iliyofuata lakini hayakuthibitisha ukubwa wa jeraha. Baadaye Real Madrid imethibitisha ukubwa wa jeraha la winga huyo.

Taarifa ya klabu

“Kufuatia vipimo vilivyofanywa leo kwa mchezaji wetu, Eden Hazard, kupitia wataalamu wa matibabu wa Real Madrid, amegundulika kuwa na jeraha kwenye misuli ya rectus femoris ya mguu wake wa kulia. Kupona kwake kutaendelea kutathminiwa” .

Tangia kuwasili Real Madrid akitokea Chelsea kwa dau la £ 88m mnamo 2019, Hazard amekuwa nje kwa jumla ya mechi 35  na idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka baada ya kutangazwa kwa pigo jingine la jeraha.

Hazard hatakuwepo kwenye mechi mbili za mwisho za Ligi ya Mabingwa, pamoja na safari kuelekea Shakhtar Donetsk.

 

FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Hazard, Eden Hazard Apata Janga Jingine!, Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa