Klabu ya soka ya Chelsea imewekewa vikwazo baada ya kufanikiwa kumsajili kiungo wa klabu ya Atletico Madrid Joao Felix kwa mkopo wa miezi sita.

Klabu ya Chelsea imefanikiwa kumsajili winga huyo wa kimataifa wa Ureno kwa mkopo wa miezi sita, Lakini klabu hiyo haijapewa nafasi ya kuweza kumsajili mchezaji huyo jumla hata akifanikiwa kuonesha ubora mkubwa katika klabu hiyo kutoka jijini London.chelseaWinga Joao Felix ameonekana jijini London mapema mchana wa leo tayari kwenda kufanya vipimo vya afya kwajili ya kujiunga katika klabu ya Chelsea. Mchezaji Felix anaongeza idadi ya wachezaji ambao wamesajiliw ndani ya klabu hiyo yenye makazi yake jijini London.

Klabu ya Atletico Madrid imeelezwa kua itahakikisha mchezaji Joao Felix anaongeza mkataba wa kusalia ndani ya klabu hiyo mpaka mwaka 2027. Hivi klabu ya Atletico inaonesha pia kuweka ugumu kwa klabu ya Chelsea kusajili mchezaji huyo.chelseaMabingwa wa zamani wa ulaya wamefanikiwa kumsajili winga huyo wa Ureno huku ikitarajiwa kufanya vizuri ndani ya klabu hiyo ambayo inaonekana kufanya vibaya kwasasa. Joao Felix atakuepo darajani mpaka mwisho wa msimu.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa