Chelsea,City Zaua Leicester Mambo mabaya.

Klabu za Chelsea, Manchester City zimefanikiwa kushinda michezo yao ya leo katika ligi kuu Uingereza huku klabu ya Leicester ikiendelea kuchechemea.

chelseaChelsea iliokua nyumbani katika dimba la Stamford Bridge imefanikiwa kupata alama tatu muhimu na magoli matatu baada ya kushinda magoli matatu kwa bila dhidi ya Wolverhampton ikiwa ni mara ya kwanza toka 2019 kuifunga timu hiyo katika ligi kuu ya Uingereza.

Magoli ya Kai Havertz,Christian Pulisic, pamoja na Armando Broja yalitosha kuwazima mbwa mwetu darajani na kuwafanya Chelsea kusogea hadi nafasi ya nne na alama zao 16.

Manchester city wao wameigaragaza klabu ya Southampton kwa mabao manne kwa bila magoli ya Joao Cancelo,Phil Foden, Riyad Mahrez huku Earling Haaland akiendeleza makali yake baada ya kufunga bao la nne la mchezo huo huku City wakikwea kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama 23.chelseaKlabu ya Leicester City yenyewe ikishindwa kutamba mbele ya Afc Bournemouth baada ya kufungwa mabao mawili kwa moja katika dimba la vitality Stadium. Leicester ambao waliicharaza Nottingham Forest kwa mabao manne kwa bila katikati mwa wiki leo wameshindwa kutamba na kuambulia kipigo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.