Conte Awaonya Washambuliaji Wake

Antonio Conte amewaonya washambuliaji wa Tottenham kwamba watalazimika kuzoea kupumzishwa kwenye mechi na mechiΒ  ikiwa klabu hiyo italazimika kuingia kwenye orodha bora ya wachezaji Duniani.

 

Conte Awaonya Washambuliaji Wake

Muitaliano huyo aliamua kuchukua nafasi ya Son na kumuweka Richarlison kwenye mechi iliyopigwa wakiwa nyumbani ambayo walikuwa wenyeji wa Leicester City baada ya Mkorea huyo kushindwa kufunga kwenye baadhi ya mechi alizopewa nafasi ya kucheza msimu huu.

Uamuzi huo ulizaa matunda mazuri kwani Son alitokea benchi na kufunga mabao matuatu (hattrick) ambapo Spurs waliibuka na ushindi mkubwa kwa kuwatandika vijana wa Brendan Rodgers mabao 6-2.

 

Conte Awaonya Washambuliaji Wake

Son amekuwa mchezaji wa kwanza wa Tottenham kufunga hattrick ya Premia League kama mchezaji aliyetokea benchi, huku akiwa ni mchezaji wa saba kufanya hivyo kwa jumla katika mashindano hayo.

Conte alisema kuwa ataendelea kuchanganya pakiti zake kadri muda unavyosonga mbele, na anataka washambuliaji wake wawe tayari kuleta matokeo pindi watakapoitwa. Conte alisema kuwa;

“Watu hawaelewi kuwa kwa kocha kusimamia hali hii siyo rahisi” Siyo rahisi kwasababu wakati mwingine unapendelea kucheza na wachezaji 13, lakini wakati fulani lazima nichukue maamuzi muhimu”.

“Wachezaji wanajua kabisa huwa nataka kushinda na kila uamuzi ni bora kwa timu, na pia kwa mchezaji bora, kuwalinda wachezaji”.

 

Conte Awaonya Washambuliaji Wake

Conte amesema kuwa ameamua kuanza mbele na Richarlison, Kane Sonny Deki, Dejan Kulusevski na pia Lucas Moura, basi kuna Bryan Gil ambaye ni matarajio mazuri .

Tottenham baada ya ,mapumziko ya Kimataifa watavaana na Arsenal ambao ni wapinzani wao wa London, kabla ya kuwatembelea Eintratch Frankfurt kwenye michuano ya Klabu Bingwa Ulaya.

Acha ujumbe