Golikipa namba wa timu ya taifa ya Ubelgiji na klabu ya Real Madrid Thibaut Courtois amesema anaamini Cristiano Ronaldo ameipa thamani ligi ya Saudia Arabia.
Nyota Cristiano Ronaldo amejiunga na klabu ya Al Nassr ya nchini Saudia Arabia wiki kadhaa zilizopita na kufanikiwa kua mchezaji anaelipwa ghali zaidi duniani. Baada ya kujiunga na klabu hiyo ya Al Nassr alifanikiwa kuongeza ushawishi na umaarufu wa timu hiyo.Golikipa Courtois amezungumza na wanahabri akiwa nchini Saudia ambapo klabu yake ya Real Madrid inacheza michuano Spanish Super Cup nchini humu “Usajili wa Ronaldo unaonesha kwa kiasi gani nchi hii inataka kukua kimichezo, Cristiano kua hapa ni maamuzi yake lakini inaonesha Saudia inataka kuimarika, Wameleta hapa kushinda Ligi”
Ni wazi golikipa Thibaut Courtois anaamini ujio wa Ronaldo kwenye ligi kuu ya Saudia Arabia utaimarisha michezo nchini humo, Lakini pia amekwenda kuikuza ligi ya nchi hiyo kutokana na nguvu ya ushawishi ambayo amekua nayo staa Cristiano Ronaldo.Kocha Ancelotti nae alizungumza kuhusu nyota Cristiano Ronaldo huku akisema “Cristiano amekua mchezaji mzuri sana, Tunamtakia kila Kheiri. Yeye ni gwiji wa klabu hii kama Gareth Bale ambaye amestaafu jana, Watakua kwenye mioyo ya wana Madrid milele”