Dalot: Tutairudisha Klabu inapostahili

Beki wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ureno Diogo Dalot ameweka wazi kua ni suala la muda tu kuirejesha klabu hiyo kwenye ubora ambao imekua nao kwa miaka kadhaa nyuma.

Diogo Dalot anaamini wako kwenye njia nzuri ya kurejea kwenye ubora wake na ni suala la muda tu kuweza kuirudisha timu hiyo kwenye zama zake ambazo ilikua nazo.dalotManchester United imekua kwenye kiwango kibovu kwa miaka takribani 10 sasa jambo ambalo limewafanya kutokushinda mataji makubwa ndani ya miaka hiyo, Jambo ambalo beki wa klabu hiyo anaamini watarudi kwenye ubora wao.

Beki huyo amekua kwenye kiwango bora ndani ya klabu hiyo tangu msimu uliomalizika na anatoa kauli kwa mara ya pili, Kwani ameshawahi kueleza kizazi hichi ndio kina nafasi ya kuirudisha klabu hiyo kwenye ubora na kukumbukwa kwenye historia ya klabu hiyo.dalotDiogo Dalot ambaye ndio beki pekee wa pembeni wa klabu hiyo ambaye hajapata majeraha mpaka sasa,Anaiona nafasi kabisa ya kuweza kuirudisha Manchester United kwenye zama zake za mafanikio.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.