Dalot Anatarajiwa Kuvaa Viatu vya Shaw

Beki wa klabu ya Manchester United raia wa kimataifa wa Ureno Diogo Dalot anatarajiwa kuvaa viatu vya beki wa kushoto wa klabu hiyo Luke Shaw ambaye amepata majeraha.

Diogo Dalot ambaye hutumika zaidi upande wa kulia lakini hutumika pia upande wa kushoto inapobidi ndie anatarajiwa kuchukua nafasi ya Luke Shaw kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Nottingham Forest.DalotMabeki wa kushoto wa klabu ya Manchester chaguo la kwanza na la pili wote wamepata majeraha ambao ni Luke Shaw na Tyrell Malacia, Hivo klabu hiyo imeamua kumtumia beki huyo wa kulia katika mchezo wao unaofuata.

Beki Diogo Dalot amewahi kutimika kama beki wa kushoto mara kadhaa licha ya kutumia mguu wa kulia na kuweza kufanya vizuri katika upande huo, Hivo haitii shaka sana kuona beki huyo anaenda kucheza upande huo wa kushoto.DalotKlabu ya Manchester United imeandamwa na majeraha siku za karibuni kwani kabla ya taarifa ya jana ya kuumia kwa beki Luke Shaw siku kadhaa nyuma ilitoka taarifa ya kuumia kiungo mpya wa klabu hiyo Mason Mount.

Acha ujumbe