David Alaba Kuikosa Gemu Supercopa

Nyota wa Real Madrid, David Alaba, yuko mbioni kukosa mechi yao ya fainali ya Supercopa ya Uhispania dhidi ya Athletic Club.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria aliikosa gemu ya ushindi wao wa nusu fainali dhidi ya Barcelona kutokana na tatizo la misuli ya paja huku Carlo Ancelotti akiwa na matumaini ya kuwa atarejea kuwa sawa.

Hata hivyo, kwa mujibu wa ripoti kutoka Marca, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 sasa anakaribia kuukosa mchezo huo na atarejea Uhispania kuendelea na matibabu yake.

Alaba Akutwa na Maambukizi ya COVID-19
David Alaba wa Real Madrid

David Alaba hajafanya mazoezi tangu alipopata jeraha wakati wa mazoezi ya kwanza ya Los Blancos mjini Riyadh na sasa kuna shaka kubwa juu yake kuelekea safari yao ya Copa del Rey kuelekea Elche katikati ya wiki.

Ancelotti tayari hana beki wa pembeni Dani Carvajal kufuatia kuthibitishwa kuwa na Covid-19 huku Jesus Vallejo pia akipambana kurejea.

Lucas Vazquez anatarajiwa kuchukua nafasi ya Carvajal katika nafasi ya beki wa kulia huku Nacho Fernandez na Eder Militao wakitarajiwa kuendelea na safu ya ulinzi wa kati kwenye fainali.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe