De Gea Kustaafu Akikosa Timu

Aliyekua golikipa wa klabu ya Manchester United David De Gea huenda akastaafu soka endapo atakosa timu ya kucheza kama golikipa namba moja katika klabu ya daraja la juu.

De Gea ambaye mkataba wake ulimalizika ndani ya Man United mwezi Juni mwaka huu baada ya msimu kumalizika na kuamua kuachana na timu hiyo, Huku mpaka sasa akiwa hajapata timu ya kucheza.de geaTaarifa zinaeleza golikipa huyo amezigomea ofa mbalimbali kutoka vilabu vya nchini Saudia Arabia, Huku akihitaji klabu ya kiwango cha juu kutoka barani ulaya ambayo hajaipata mpaka wakati huu.

Golikipa huyo raia wa kimataifa wa Hispania inaelezwa alikua kwenye orodha ya magolikipa wanaotakiwa na klabu ya Real Madrid baada ya golikipa namba moja wa klabu hiyo Thibaut Courtois, Lakini kocha Ancelotti alimuhitaji zaidi Kepa kutoka klabu ya Chelsea.de geaDavid De Gea amecheza kwa mafanikio makubwa sana ndani ya klabu ya Manchester United kwa takribani miaka 12 na kuachana na timu hiyo mwaka huu, Huku mpaka sasa hakuna timu ambayo imemsajili na ikiendelea hivi basi golikipa huyo atatundika daluga.

Acha ujumbe