Declan Rice; Huku United, Kule Chelsea.

Maneno ya waswahili yanamaana kubwa ndani yake. Walisema, ‘kizuri chajiuza’. Ukihusianisha na Declan Rice, huu msemo unaukweli ndani yake.

Baada ya kuendelea kufanya vyema katika safu ya kiungo ndani ya West Ham United, Declan Rice anagonganisha timu mbalimbali zinazopigana vikumbo kuitafuta sahihi yake.

Kwa sasa Rice amekabidhiwa majukumu ya unahodha wa kikosi hicho cha “Wagonga nyundo wa London” na anayatumikia vyema katika nafasi yake kama kiungo mkabaji wa timu hiyo.

Uwapo na Declan Rice kwenye timu yako, hunashaka ya ulinzi thabiti kwa mabeki wa timu yako kwani ni mchezaji mwenye uwezo na nidhamu kubwa ya kucheza katika nafasi hiyo.

Rice (kulia) akipambana na Adama Traore (kushoto)

Manchester United kupambana na Chelsea katika kuiwania sahihi ya kiungo huyu raia wa Uingereza ambaye bado anamkataba wa kuitumikia West Ham United mpaka Juni 2024.

Kuna taarifa zilianza kusambaa kuwa Rice anafanyajitihada za kurejea Chelsea ambapo alikulia pale kabla ya kuondoka akiwa na miaka 14. Frank Lampard ni shabiki mkubwa wa Rice na alitakakumsajili majira ya kiangazi yaliyopita japo hakufanikiwa.

Huenda Lampard akafanya kweli kwenye dirisha la usajili lijalo mapema mwezi Januari. Endapo Chelsea watavuta muda mpaka majira ya kiangazi mwakani -2021, watakuwa wameingia vitani na United ambayo inatajwa kuwa na mpango wa kuweka pesa mezani kwa ajili ya Rice ifikapo Juni 2021.

Hapa kutahitajika nguvu ya ziada kwenye suala zima la pesa kwani Declan Rice hatouzwa kwa pesa ndogo kutokana na urefu wa mkataba wake na West Ham, lakini pia mapenzi binafsi ya mchezaji yataamua ni timu gani ataitumikia baada ya msimu huu.

Unadhani Rice ataichagua timu gani kati ya zinazoiwania sahihi yake kwa udi na uvumba?


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

19 Komentara

    Akitua man u itapendeza zaid

    Jibu

    Declan Rice ni mchezaji mzuri na ananidhamu uwanjani

    Jibu

    Declan Rice nimchezaji mzuri anajitahidi kwakweli

    Jibu

    Rice yupo vizuri ndiomaana klabu zinamgombania

    Jibu

    United itamtwaa

    Jibu

    Nic

    Jibu

    Safii

    Jibu

    untd

    Jibu

    Safi

    Jibu

    gud

    Jibu

    Yupo vizuri akitua kwenye timu yoyote hile itakuwa poa sana

    Jibu

    Nice

    Jibu

    👏👏👏👏

    Jibu

    Raja sanaaa

    Jibu

    Kiungo mzur

    Jibu

    Habar nzur

    Jibu

    Upendapo nendaa tu

    Jibu

    Kweli kizuri kinajiuza

    Jibu

    Ni mchezaji mzuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.