Diomande Awekewa Bei ya Kutisha, RB Leipzig Wafunga Mlango

Klabu ya RB Leipzig imeanza mkakati mzito wa kumbakisha nyota wao chipukizi , Yan Diomande, kwa kumpa mkataba mpya utakaokuwa na masharti magumu kwa klabu zinazomtaka, ikiwemo Liverpool. Lengo kubwa ni kuhakikisha wanaendelea kuwa na udhibiti kamili juu ya mustakabali wa mchezaji huyo mwenye miaka 19.

Diomande Awekewa Bei ya Kutisha, RB Leipzig Wafunga Mlango

Taarifa zinaeleza kuwa Leipzig wanataka kuondoa kabisa kipengele cha release clause katika mkataba mpya, hatua itakayozuia timu yoyote kununua mchezaji huyo kwa bei iliyowekwa moja kwa moja. Badala yake, klabu yoyote italazimika kukaa mezani na Leipzig na kujadiliana, kitu kinachowapa nguvu kubwa ya kupanga bei watakayotaka.

Mbali na hilo, Diomande anatarajiwa kuongezewa mshahara mkubwa kulingana na kiwango chake bora alichoonyesha msimu huu. Hii ni njia ya kumshawishi kubaki, licha ya presha kubwa kutoka kwa vilabu vikubwa barani Ulaya vinavyomfuatilia kwa karibu.

Diomande Awekewa Bei ya Kutisha, RB Leipzig Wafunga Mlango

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Hata hivyo, Leipzig wameweka wazi kuwa hawatafunga kabisa mlango wa mauzo lakini kwa masharti magumu. Inasemekana dau la kuanzia euro milioni 100 ndilo litakalofungua mazungumzo, kiwango ambacho kinaweza kuwakatisha tamaa wengi, isipokuwa matajiri wakubwa wa soka duniani.

Diomande Awekewa Bei ya Kutisha, RB Leipzig Wafunga Mlango

Kwa sasa, uamuzi uko mikononi mwa Diomande. Kubaki Leipzig kunamaanisha kuendelea kukua katika mazingira tulivu, lakini bila uhuru wa kutoka kirahisi. Kuondoka, kwa upande mwingine, kunaweza kumpa jukwaa kubwa zaidi mapema.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.