Dirk Kuyt: Man Utd Watakuwa Wamepata Kocha Bora ikiwa Watampa kazi Ten Hag

Mchezaji wa zamani wa klabu ya Liverpool Dirk Kuyt anaamini kuwa Man Utd watakuwa wameokota dodo kwenye mpera ikiwa tu watampa kazi Erik Ten Hag kama kocha atakayerithi mikoba ya kocha wa muda Ralf Rangnick.

Klabu ya Man Utd kwa sasa ipo kwenye mchakato wa kutafuta kocha ambaye atarithi mikoba ya kocha wa muda Ralf Rangnick ambaye mwisho wa msimu anaena kuwa mkurugenzi wa ufundi.

Dirk Kuyt
Dirk Kuyt

Dirk Kuyt akizungumza na waandishi alisema, “Ten Hag ni kocha bora, mwenye uzoefu, tayari amaejifunza vya kutosha, amefanya kazi kwenye klabu ya Bayern Munich kama kocha msaidizi, baadae  Utrech na sasa Ajax.

“Ni kocha bora  ambaye ameijimarisha sana, ndani na nje ya uwanja. Najua kuna watu wanawasiwasi na uzungumzaji wake wa lugha ya kingereza, jinsi anavyozungumza mbele ya kamera, lakini unaona jinsi anavyoimarika siku hadi siku kama kocha na nadhani anaweza kuwa kocha bora kwenye timu yoyote kubwa barani ulaya.

“Mbinu zake, jinsi anavyofikilia kuhusu mpira, inavutia, na itakuwa vizuri kama atapata nafasi ya kufundisha timu kubwa.”

Ten Hag ni moja ya chaguo linalopigiwa upatu kuweza kuchukua mikoba ya kuino a klabu ya Man Utd akiwemo pamoja na Mauricio Pochettino, Luis Enrique na Julen Lopetegui


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe