Baada ya kuona mchezaji wao anaviziwa sana na klabu nyingi sasa klabu ya soka ya Borussia imekuwa sio mbinafsi kwa kuweka mezani bei ya mchezaji wao kwa yeyote atakayehitaji kuwa naye wakati wowote ule maana wameona ikiendelea hivyo watakosa soko mapema.
Mchezaji Sancho amekuwa na kiwango cha pekee katika umri wake kwa kuwatamanisha miamba wengi wa soka kuhitaji huduma yake kutokana na uwezo wake na umri wake kuwa rafiki kwa kufanya makubwa sana siku za usoni. Kama alivyoanza kuaminiwa tayari kwenye timu ya taifa na klabu yake ya Dortmund ambayo imepiga hatua sana msimu huu pamoja na kupotea kidogo kwenye uwiano waliouanza hapo awali.
Baada ya Manchester United kuonesha nia ya dhahiri kabisa juu ya kuhitaji mchezaji huyo atue Old Trafford wameamua kuanika bei yake kuwa ni £100m ili kama bado watavutiwa naye waandae kiwango hicho cha fedha kusudi waweze kumnasa na wao waweze kutumia malipo hayo kutafuta mbadala wa mchezaji huyo.
Nyota huyo alijiunga na Westfalenstadion mwaka 2017 baada ya kukosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha Manchester City kwa uhamisho wa £7m ikiwa alikuwa na kiwango cha pekee sana hata kwa kipindi hicho lakini kutokana na sintofahamu kikosini hapo aliamua kutimka ili kutafuta eneo ambalo angepata mbadala wa kucheza zaidi.
Sancho ameonesha makali yake katika mwaka wa kwanza tu klabuni hapo baada ya kujiunga nao kwa kuweza kudhihirisha ubora wake wa kufunga magoli tisa na kutoa pasi zisizopungua 17 katika mashindano yote; hayo yote yakiwa ni mafanikio aliyoyapata ndani ya muda mfupi sana na kwa umri ambao bado unampa nafasi ya kuendelea kuudhihirishia ulimwengu kwamba anaweza.
Nyota huyo mwenye miaka 18 amewashangaza wengi kwa uwezo wake lakini pia anaendelea kujenga historia yake ndani ya michuano hiyo. Lakini pia kwa upande wake anavutiwa na kuliendeleza soka lake mbele zaidi hata kwa kujiunga na klabu nyingine zaidi ya aliyopo ili aweze kujenga wasifu wake zaidi katika umri wake mdogo.
Dortmund pia wanaonekana kimbilio la wengi kwa sababu hata sasa wameweza kuwauzia Chelsea nyota wao Christian Pulisic kwa ada ya £57m; lakini pia waliweza kufanya biashara kubwa na Barcelona juu ya Ousmane Dembélé lakini msimu uliopita pia walifanya biashara na Arsenal juu ya kuwauzia Pierre-Emerick Aubameyang hivyo kwa aina hiyo ya mauzo bado vibubu vyao vina chochote kitu.
Wawe makini…
Kutokana na hilo bado wana nafasi ya kuvunja akaunti zao na kuamua kufanya usajili wowote watakaoona unawafaa wao. Lakini suala la msingi wanapaswa kuwa makini maana wanaweza kufanya biashara ambayo wao wakashindwa kuirudisha kwenye ramani yake.


Mariam mtandama
Anakipaji sana
Rehema
Safi
devotha
sancho ni mchezaji mzuri sana kila timu inatamani imchukue