Wakati huu ambao ni dhahiri, Paulo Dyabala hana muda mrefu ndani ya kikosi cha Juventus, huenda mchezaji huyu akabadilisha upepo ndani ya Serie A?

Ilitokea kwa Zlatan Ibrahimovic, Arturo Vidal, Chiellini na huenda – Paulo Dyabala akawa ni miongoni mwa wachezaji waliobadilisha upepo ndani ya ligi soka nchini Italia.

Paulo na Juve wameshindwa kufikia makubaliano ya kusaini mkataba mpya na hivyo, pande zote zimefikia tamati ya majadiliano ambapo ni wazi sasa, Paulo ni mchezaji huru kuanzia Juni 30, 2022.

Kwa alipo sasa hivi, anaruhusiwa kufanya mazungumzo na kusajiliwa (kwa mkataba wa awali) na timu yeyote nje ya Serie A lakini, huenda akachagua kubaki kwenye ligi hiyo ila akiwa kwenye timu pinzani dhidi ya Juventus.

Dyabala, Dyabala Atabadili Upepo Serie A?, Meridianbet

Inasemekana, kumekua na minong’ono huenda Lautaro Martinez akaondoka Inter na kujiunga na Atletico Madrid kitu ambacho kitawafanya Inter kuingia sokoni kumtafuta mbadala wake.

Hapa ndipo jina la Paulo linapotajwa na, huenda hilo likatokea baada ya msimu huu kumalizika tena bila kiasi kikubwa cha pesa kutumika kukamilisha hili.

Hata hivyo, Dyabala bado anahusishwa na vilabu vingine barani ulaya ikiwemo Tottenham Hotspur, Arsenal na Man United ambao wamekua wakitajwa kwa muda mrefu sasa.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa