Kocha wa Italia Roberto Mancini amejikuta katika wakati mgumu Baada ya taifa hilo kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia 2022 na mama wa kocha huyo wa zamani wa Manchester City huenda akahitaji majibu yanayo eleweka kwanini mchezaji Mario Balotelli hakuitwa katika kikosi cha timu ya taifa.
Mama wa Mancini anaamini Balotelli angeisadia timu hiyo sababu ya uimara aliyonao hakuna ambaye angemzuia asifunge pia alilaumu Jorginho kukosa penati kadhaa ambazo zingeamua Italia kufuzu kwenye makundi.
Akiongea na Rai Radio 1 Marianna Puolo alisema: “Mchezo ulikuwa mikononi mwetu lakini ushambuliaji ulikuwa dhaifu.” alisema mama wa Mancini
“Ningekuwa ni mimi ninge muita Balotelli sababu ana nguvu na huwa hana mzaha mbele goli.”
“Ndiyo Kuna wakati anafanya vitu vya kijinga lakini ningemuita hivyohivyo.
Italia imeshindwa kufuzu kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo baada kuzikosa fainali hizo mwaka 2018 huko Urusi ambapo bingwa alikuwa ni Ufaransa.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.