Ederson: Ana Imani Ancelotti Ataifundisha Brazil

Golikipa wa klabu ya Manchester City Ederson Moraes ameonesha ana imani kubwa kua kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti atakinoa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil siku za usoni.

Ederson akiongea na waandishi wa habari akiwa kwenye kambi ya timu ya taifa ya Brazil anasema ameongea na wachezaji wenzake ambao wana ukaribu na kocha huyo Eder Militao, Vinicius Jr, na Casemiro na kusema kuna uwezekano mkubwa kocha huyo akaifundisha timu ya taifa ya Brazil.edersonGolikipa huyo aliongezea kwa kusema watajitahidi kwa kiasi kikubwa kuhakikisha wanaitoa Real Madrid kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ili kocha huyo ajiunge na kikosi hicho haraka iwezekanavyo, Kutokana na kauli ya kipa huyo inaonesha kuna uwezekano mkubwa Ancelotti akawa kocha mpya wa Brazil.

Kocha Ancelotti anazungumzwa sana kuchukua mikoba ya Tite na kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, Taarifa za ndani kutoka ndani ya klabu ya Real Madrid zinaeleza kua kocha Ancelotti anaweza kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.edersonKocha Ancelotti amekua kwenye wakati mgumu sana ndani ya klabu ya Real Madrid siku za karibuni haswa kwenye michuano ya kombe la ligi kuu nchini humo, Kitu kinachoweka ajira yake rehani ndani ya Real Madrid na kuweka urahisi mkubwa wa kujiunga na Brazil jambo ambalo Ederson anaona likitokea siku za usoni.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.