Kiungo wa zamani wa vilabu vya Schalke 04, Weder Bremen, Real Madrid, na Arsenal Mesut Ozil ametangaza kustaafu soka la ushindani mapema leo baada ya kutumikia soka kwa kipindi kirefu na mafanikio makubwa.
Mesut Ozil ametangaza kustaafu soka akiwa anaitumikia klabu ya Instanbul Basaksaher ya nchini Uturuki baada ya kutoka klabu ya Fenerbahce, Mchezaji huyo ametangaza kustaafu baada ya kufanya mambo makubwa katika ulimwengu wa soka.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani ametumia mitandao yake ya kijamii kutoa taarifa hiyo huku akizishukuru timu zote ambazo amewahi kuzitumikia, Bila kuwasahau wachezaji wenzake ambao amewahi kucheza nao katika vilabu hivo alivyovitumikia kwa wakati akicheza soka.
Mesut Ozil atakumbukwa kama moja ya viungo hodari sana kuwahi kutokea kwenye ulimwengu wa soka akiwa na uwezo mkubwa sana wa kupiga pasi za mwisho, Vilevile kwenye uwezo wake wa kuweza kucheza kama namba 11 pale ambapo atakua hatoki katikati ya uwanja kama namba 10.
Kiungo Mesut Ozil amepata mafanikio mengi akiwa na vilabu vyake alivyowahi kuvitumikia kwa wakati wote ambao amecheza soka, Lakini kiungo huyo alikua akiitumikia timu ya taifa ya Ujerumani kwa kipindi kirefu na kufanikiwa kutwaa taji la kombe la dunia mwaka 2014 huku akiwa kama mchezaji muhimu zaidi kwenye kikosi hicho.

