Rabiot Hajajua Hatma Yake Juventus

Kiungo wa kimataifa wa Ufaransa Adrien Rabiot mpaka sasa hajajua hatma yake ndani ya klabu ya Juventus kwani mkataba wa kiungo huyo unamalizika mwisho wa msimu huu.

Rabiot ambaye alikua amejiunga na klabu hiyo akitokea klabu ya PSG ya nchini Ufaransa amekaribiua kumaliza mkataba ndani ya wababe hao wa soka nchini Italia, Lakini mchezaji huyo ameweka wazi kwasasa anawaza zaidi kumaliza msimu klabuni hapo.rabiotKiungo Adrien Rabiot alikaribia kujiunga na klabu ya Manchester United mwishoni mwa dirisha kubwa lililopita, Lakini dili hilo halikufanikiwa kukamilika na kulzimika kubaki ndani ya Juventus ambapo mkataba wake unafika ukingoni mwisho wa msimu huu.

Kiungo huyo wa kimtaifa wa Ufaransa anawindwa na vilabu mbalimbali barani ulaya lakini vilevile klabu ya Juventus inafikiria kumpa mkataba mpya ili aendelee kusalia ndani ya viunga vya Turin misimu mingine inayofuta mbele, Huku yeye pia akiweka bayana lolote linawezekana.rabiotRabiot kuhusu mustakbali wake ndani ya Juventus amesema anaweza kuondoka ndani ya timu hiyo au kusalia vilevile, Hivo ni wazi kiungo huyo amefungua milango wazi kwa wababe hao wa soka nchini Italia kwakua amekiri ana furaha ndani ya klabu hiyo kwasasa hivo kama ofa itakuja nzuri atasaini mkataba mpya ndani ya timu hiyo.

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.