Elliot Apata Majereha

Kiungo wa klabu ya Liverpool raia wa kimatiafa wa Uingereza Harvey Elliot amepata majeraha ambayo yatamuweka nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja nusu kutokana na taarifa iliyotoka.

Elliot amepata majeraha kwenye mguu wake ambapo atakua nje ya uwanja mpaka mwishoni mwa mwezi wa kumi, Hivo klabu yake ya Liverpool ambayo itakua inamkosa kwenye michezo yote ambayo itakua inapigwa kwenye kipindi hiki ambacho amepata majeraha kiungo huyo.elliotWachezaji wengi wamekua wakipata majeraha hivi karibuni kwenye michuano ya kimataifa licha ya Elliot kutopata majeraha yake kwenye michuano ya kimataifa, Lakini wachezaji kadhaa wamepata majeraha kwenye michuano ya kimatiafa ambayo ilikua inaendelea wiki mbili hizi.

Ndani ya klabu ya Liverpool mchezaji ambaye amepata majeraha siku za karibuni ni Harvey Elliot lakini vilabu vingine kama Arsenal vimeandamwa na majeraha kwelikweli, Kwani mchezaji muhimu ndani ya kikosi hicho nahodha Martin Odegaard amekubwa na majeraha akiitumikia timu yake ya tiafa ya Norway.

Acha ujumbe