Kulikua na upepo mbaya unaopepea kuelekea Newcastle United, hatimaye wamepata ushindi kwenye EPL.
Newcastle United wamekuwa na msimu mgumu kwenye EPL mpaka sasa. Matokeo mabovu yalimuondoa Steve Bruce na benchi lake la ufundi. Ujio wa Eddie Howe ukaleta matumaini mapya kwa mashabiki na uongozi mpya wa klabu. Bado, matokeo yaliendelea kuwa yale yale.
Wikiendi hii, The Magpies walikuwa St James’ Park kuchuana na Burnley. Timu zote zipo kwenye nafasi za kushuka daraja msimu huu, hali ni mbaya zaidi kwa Newcastle ambao ni wanashika nafasi ya pili kutoka mkiani.

Kwa mara ya kwanza baada ya michezo 15 ya Ligi Kuu soka nchini Uingereza, Callum Wilson anapachika goli lake la 6 na goli pekee linalowapa ushindi wa kwanza Newcastle United.
Kinachonogesha msimu huu ni kwamba, timu tatu za chini, zote zinapointi 10 mpaka sasa. Mambo yanazidi kunoga!!
Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.


