Thomas Tuchel: Hatupaswi Kuendelea Kukosea

Kocha mkuu Thomas Tuchel amekiri kwamba Chelsea hawapaswi kuendelea kufanya makosa baada ya kichapo cha 3-2 kutoka kwa West Ham United.

Licha ya The Blues kuongoza mara mbili, makosa ya kipa Edouard Mendy yaliwazawadia West Ham penalti, huku mlinda mlango wa Senegal kuzuia mpira wa krosi wa Arthur Masuaku kuingia ndani ya lango.

Licha ya juhudi za kuusaka ushindi, na makosa ya wazi kutoka kwa Mendy, Chelsea ilifanya makosa mengine kadhaa kama timu, jambo ambalo Tuchel alilitaja kwa haraka baada ya kumalizika kwa mechi.

Thomas Tuchel
Thomas Tuchel

“Sidhani kama tulicheza vibaya, mechi ilikuwa sawa, tunaweza kushinda kwa uchezaji huu.”

“Ni ngumu kucheza hapa, tulifanya makosa mengi ya binafsi. Tayari tulifanya dhidi ya Manchester United na Watford na tukaadhibiwa – ikiwa unataka matokeo katika kiwango hiki lazima upunguze makosa.”

Akizungumzia penalti ya kipindi cha kwanza, Mjerumani huyo aliongeza: “Kila mtu anahusika, pasi si uamuzi bora, mwelekeo si bora, tunaweza kulinda lakini maamuzi pia hayakuwa bora kwa Edu katika hili.”

Chelsea itashuka hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League ikiwa Manchester City na Liverpool wataweza kuwachapa Watford na Wolverhampton Wanderers mtawalia.


MUDA WA KUJIACHIA NA CARNAVAL JACKPOT

Mabingwa Meridianbet hawajawahi kukuacha mnyonge hasa katika kipindi hiki cha msimu wa sikukuu, kasino maridhawa ya Carnaval Jackpot inakupa thamani ya dau lako. Kuwa mmoja wa washindi leo hii.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.