Klabu ya Everton ina maamuzi ya kufanya kwenye dirisha hili la usajili. Richarlison na Moise Kean, nani anatoka- nani anabaki?
Imeripotiwa kuwa Carlo Ancelotti ameilekeza Real Madrid kumsajili Richarlison kwenye dirisha hili la usajili. Richarlison alisajiliwa na Marco Silva (2017) alipokuwa kocha wa Watford wakati ule mchezaji huyo alikuwa Fluminense (Brazil). Baada ya Silva kupewa kibarua cha Everton, alimsajili Richarlison kwa dau la £47M ambapo alikaa klabuni hapo mpaka Ancelotti alipokuja.
Richarlson alikuwa kipenzi cha Ancelotti na sasa kocha huyo anataka kumsajili mshambuliaji huyo ili wakaendelee kufanya kazi pamoja pale Santiago Bernanbeu. Swali ni Je, Rafa Benitez atakubali kumuachia Richarlison?

Moise Kean alitolewa kwa mkopo na klabu hiyo na kwenda kucheza PSG, akiwa Paris alipata nafasi ya kuonesha uwezo wake wa kuzifumania nyavu katika mashindano makubwa ikiwemo Ligi ya Mabingwa. Ripoti zinasema, Kean hatotolewa klabuni hapo msimu huu na yupo kwenye mipango ya Benitez kuelekea kwenye msimu mpya wa EPL.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!

