Muendelezo wa mashindano ya Wimbledon 2021 unaendelea kutoa matokeo ya kila namna ikiwa ni hatua ya robo fainali kwa wanaume. Roger Federer apoteza mchezo mwanzo mwisho.
Federer alikuwa uwanjani akichuana na Hubert Hurkacz katika mchezo wa robo fainali ikiwa ni harakati za kulisaka taji lake la 9 la Wimbledon. Mambo yalimuendea kombo baada ya kukubali kipigo cha seti 6-3 7-6 (7-4) 6-0 na Hurkacz kufuzu hatua ya nusu fainali ya Grand Slam kwa mara ya kwanza.
Ushindi wa Hurkacz unampatia nafasi ya kuchuana na Matteo Berrettini kwenye hatua ya nusu fainali.
Bingwa mtetezi wa mashindano haya, Novak Djokovic ameonesha ukomavu wake katika mchezo wa tenesi na ubora wake ulimzidi uwezo Marton Fucsovics.
Djokovic ameibuka kidedea baada ya kumaliza mchezo kwa matokeo ya seti 6-3 6-4 6-4 na sasa atachuana na Denis Shapovalov kwenye nusu fainali ijumaa hii.
IcyGems kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet. Ndio, ukiwa kwenye nyumba ya mabingwa, ndipo utakapoufurahia ubora wa Kasino ya Mtandaoni sambamba na kushinda kwa ushindi mkubwa! Ishi na hii, IcyGems!